Alisi Ndani YA Nchi YA Ajabu: Alice's Adventures in Wonderland in Swahili, Paperback/Lewis Carroll

Alisi Ndani YA Nchi YA Ajabu: Alice's Adventures in Wonderland in Swahili, Paperback/Lewis Carroll

Editura
An publicare
2015
Nr. Pagini
160
ISBN
9781782011224

Descriere

Lewis Carroll ni jina la uandishi: Charles Lutwidge Dodgson ndilo jina halisi la mwandishi wa kitabu hiki, na alikuwa mhadhiri wa hisabati huko Christ Church, Oxford. Dodgson aliianza hadithi hii tarehe 4 Julai mwaka 1862, pale alipofanya matembezi katika mashua ya makasia huko Oxford katika mto Thames akiwa pamoja na Mchungaji Robinson Duckworth, Alice Liddell (aliyekuwa na miaka kumi), binti wa Mkuu wa kitivo huko Chirst Church, pamoja na dada zake wawili Lorina (aliyekuwa na miaka kumi na mitatu), na Edith (aliyekuwa na miaka minane). Kama inavyoonekana wazi katika shairi pale mwanzoni mwa kitabu, mabinti hawa watatu walimwomba Dodgson awahadithie hadithi, na kwa kusita sita akaanza kuwahadithia ile hadithi ya awali. Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa huko Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Somalia na nchi nyingine zilizo jirani na nchi hizi za Afrika ya mashariki. Kiswahili kimekirimu tafsiri za kigeni kwa karne nyingi na pia tafsiri imekuwa na jukumu muhimu la kukuza lugha hii kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Pia katika karne ya 19, tafsiri ilikuwa ndiyo chanzo cha riwaya ndani ya fasihi ya Kiswahili, hivyo imeweza kuathiri waandishi muhimu. Tafsiri hii ni ya kifasihi zaidi, pia imelengea kiuaminifu zaidi hadithi ya awali. "Alisi" ilitafsiriwa kwa mara ya kwanza mwaka 1940 ambapo mfasiri alifupisha hadithi hiyo na kuiita "Elisi katika Nchi ya Ajabu." Pia alimgeuza mhusika mkuu kuwa mtoto wa Kiafrika aliyemwita Elisi. Hii tafsiri mpya iliyofanywa na Ida Hadjivayanis, imetolewa kama mojawapo ya kazi zinazosherehekea kuazimia kwa miaka 150 tangu kuchapishwa kwa toleo la kitabu hiki la mwaka 1865. Tafsiri hii itamwezesha msomaji wa 'Alisi' wa Kiswahili apate hisia zilizokusudiwa na mwandishi hapo awali. --- Lewis Carroll is a pen-name: Charles Lutwidge Dodgson was the author's real name and he was lecturer in Mathematics in Christ Church, Oxford. Dodgson began the story on 4 July 1862, when he took a journey in a rowing boat on the r

Pe aceeași temă

Lewis Carroll